Julius na Aroni

Julius na Aroni (walifariki Caerleon, leo nchini Wales, 304 hivi) walikuwa Wakristo waliouawa katika dhuluma wa kaisari Diokletian[1].

Kabla yao aliuawa Albano, halafu wengine wengi kwa ukatili mkubwa.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 22 Juni[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/58970
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy